Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shida ya maji kwa wanawake wa Senegal yasalia historia

Mradi pia unahusisha uvunaji wa maji
UNDP Rwanda/Gabrielle Tillberg
Mradi pia unahusisha uvunaji wa maji

Shida ya maji kwa wanawake wa Senegal yasalia historia

Wanawake

Mradi mpya wa shirika la chakula na kilimo duniani FAO, wa kukusanya na kuhifadhi maji katika matangi makubwa yaliyochimbiwa ardhini umesaidia wakulima wanawake wanaoishi maeneo yenye ukame nchini Senegal.

 Mmoja wa wanawake hao ni Guile Mane mwenye umri wa miaka 39 ambaye amesema kwa muda mrefu amehangaika wakati wa kiangazi na hata mvua ikinyesha ni kwa kiwango kidogo.

Uhaba wa maji ulisababisha mimea kukauka, hakuna chakula na yeye na wanawake wengine walitembea muda mrefu kusaka maji na hata kulazimika kutumia fedha kidogo walizo nazo kununua huduma hiyo.

 “Watoto walihara kwa sababu chakula walichokula kilisababisha waugue. Baadhi ya wanawake walishindwa kuwatunza watoto wao walipougua. “Mchicha tulionunua sokoni nao ulioza ndani ya siku mbili na pia ulikuwa na kemikali nyingi.”

Kilio cha Guile na wenzake kilisikilizwa na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO ambalo kupitia mradi wake wa matangi milioni moja ya maji ukanda wa Sahel, wenye lengo la kusaidia familia zilizoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi, sasa Guilé na wenzake wana huduma ya maji.

“Tangi hili lina  manufaa sana. Mapato yote tuliyopata kabla ya  ujenzi wa tangi hili yametumika kulipa Ankara za maji.  Kwa kuwa tuna hili tangi, tunamwagilia mashamba yetu maji mengi bila malipo.”

Mpango huo umezisaidia sana familia za vijijini kuzidisha kile wanacholima kwa ajili ya kuboresha lishe kama vile mboga za majani, pamoja na kuongeza pato lao na hivyo kuwa na afya bora.

Wanawake hao wameunda kikundi cha ushirika ambapo kila