Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia na mashambulizi sio suluhisho Somalia: Guterres

Mpiganaji wa zamani wa Al-Shabab akiwa katika kituo cha kubadili tabia cha mjini Baidoa
Guy Oliver/IRIN
Mpiganaji wa zamani wa Al-Shabab akiwa katika kituo cha kubadili tabia cha mjini Baidoa

Ghasia na mashambulizi sio suluhisho Somalia: Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali mashambulizi ya mabomu mawili yaliyotokea  Baidoa nchini Somalia.

Katika taarifa iliyotolewa  mwishoni mwa juma na msemaji wake mjini New York nchini Marekani, Antonio Guterres, amelaani vikali mashambulizi hayo na kutoa salam za rambirambi kwa ndugu na jamaa za walioathirika na mkasa huo na kuwaombea ahuweni ya haraka wotewaliojeruhiwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Bw Guterre amekariri uungaji mkono pamoja na mshikamano wa Umoja wa Mataifa na watu pamoja na serikali ya Somalia.

Ameongeza kuwa anaamini kwamba ghasia za kila mara pamoja na mshambulizi ya kiholela hayatawavunja nguvu watu wa Somalia katika jitihada zao ya kutafuta amani na utengamano.

Na wakati huohuo, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia na Mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNSOM, Nicholas Haysom, ameonyesha mshikamano wake katika kumbukumbu ya shambulizi la kujitoa  mhanga  lililofanyika mwaka mmoja uliopita  mjini Mogadishu.

 

Magari  yaliyoharibika kufuatia mashambulio mawili ya kujilipua yaliyofanywa na Al Shabaab nchini Somalia na kusababisha vifo vya makumi kadhaa ya watu.
UN /Stuart Price
Magari yaliyoharibika kufuatia mashambulio mawili ya kujilipua yaliyofanywa na Al Shabaab nchini Somalia na kusababisha vifo vya makumi kadhaa ya watu.


Bw Haysom amekumbusha athari zinazotokana na vifaa vya kujilipua kwa raia lakini vilevile kwa jamii nzima. Na amesema hakuna sheria, hatua ,sababu wala chochote kinacho halalisha vitendo hivyo vya kigaidi ambavyo vinakatili maisha ya watu wengi wasio na hatia.


 Shambulio hilo lilisababisha vifo vya watu 587 na kuwajeruhi wengine 316.