Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNSOM ahimiza ushirikiano katika kuleta maendeleo Somalia

Bwawa la maji lililojengwa na moja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa , UNDP kwa ushirikiano wa wizara ya mazingira ya Somalia kwa ajili ya kuwasaidia wakazi wa Puntland Somalia na majimbo ya jirani
undp Somalia
Bwawa la maji lililojengwa na moja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa , UNDP kwa ushirikiano wa wizara ya mazingira ya Somalia kwa ajili ya kuwasaidia wakazi wa Puntland Somalia na majimbo ya jirani

Mkuu wa UNSOM ahimiza ushirikiano katika kuleta maendeleo Somalia

Amani na Usalama

 

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa mpango wa Umoja wa Matyaifa nchini Somalia UNSOM, James Swan leo amezuru jimbo la Kusini Magharibi na kuchagiza mshikamano ili kufanikisha juhudi za kuleta amani ya kudumu katika taifa hilo la pembe ya Afrika.

Akiwa katika mji mkuu wa jimbo hilo Baidoa Bwana Swan amekutana na Rais Abdiaziz Hassan Mohamed ‘Laftagareen.’ Na kujadili njia mbalimbali ambazo UNSOM na jimbo hilo wanaweza kushirikiana kuleta athari chanya katika maisha ya wakazi eneo hilo.

Swan ameushukuru uongozi wa jimbo hilo “Namshukuru Rais Laftagareen kwa kunipokea leo Baidoa ambapo nimekuja kwa ajili ya kuimarisha ushirika wetu kuhusu masuala ya kisiasa, kuwajengea uwezo na shughuli za kibinadamu. Na pia kuwaambia watu wa jimbo la Kusini Magharibi kwamba familia ya Umoja wa Mataifa inafanya kila njia kukidhi mahitaji yao hivyo ili tuwekze kuwa na matokeo chanya katika changamoto mbalimbali ambazo zinalikabili jimbo hili kwa lengo la kujenga kwa pamoja taasisi ambazo ni imara na wanazistahili watu wa jimbo hili.”

Swan amesisitiza umuhimu wa kusaidia katika shughuli za kijamii zinazoendeshwa na serikali , ofisi ya Umoja wa Mataifa , mashirika ya Umoja wa Mataifa  na mpango wa Muungano wa Afrika nchini Somalia.

UNSOM inalisaidia jimbo hilo katika miradi mbalimbali ya muhimu ikiwemo ujenzi wa kituo cha msaada wa kuwajumuisha katika jamii wajumbe wa zamani wa makundi yenye itikadi kali, kuwahamisha wakimbizi wa ndani, na kufungua kituo maalum cha mpito na kuimarisha brabraza za biashara baina ya Moghadishu na Baidoa ambayo inatarajiwa kuchangia uchumi wa jimbo hilo.

Mwakilishi huyo maalum wa Umoja wa Mataifa Somalia amesisitiza jinsi gani uhusiano mzuri kati ya serekali ya shirikisho nay a jimbo endapo utaimarishwa  na kuwa na msingi imara wa taasisi zake , pamoja na watu kuheshimu sharia . “Tunatumai kwamba uhusiano mzuri baina ya sewrikali ya shirikisho ya Somalia na wajumbe wa serikali hiyo unaweza kuchangia kuwa na mfumo bora unaofanya kazi wa shirikisho.”