Nimefika Somalia, nimejionea na sasa ni kuchukua hatua- Mshauri wa UN
Somalia! Somalia! Somalia! Kila uchao changamoto zinazidi kukumba wananchi wake kutokana na sio tu ukosefu wa usalama katika baadhi ya maeneo, bali pia madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Hivyo ni vichocheo vya mamia ya maelfu ya watu kukimbia makwao na kusalia wakimbizi wa ndani.