Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pongezi Sudan Kusini kwa kutia saini mkataba wa Amani:Guterres

Mwanamke akichora kwenye ukuta maandishi yanayosema amani, katika mji wa yei
UNMISS/Denis Louro
Mwanamke akichora kwenye ukuta maandishi yanayosema amani, katika mji wa yei

Pongezi Sudan Kusini kwa kutia saini mkataba wa Amani:Guterres

Amani na Usalama

Mkataba wa Amani uliotiwa saini na pande mbili hasimu katika mgogoro unaoendelea nchini Sudan Kusini umepongezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisema “hiyo ni hatua muhimu”katika kuelekea kukomesha mgogoro huo.

António Guterres amethibitisha wajibu wa Umoja wa Mataifa katika kusaidia kufikia makubaliano ya amani yaliyo ya haki na endelevu kwa nchi hiyo.

Sudan Kusini ilipata uhuru mwezi Julai 2011, na kuifanya kuwa taifa change kabisa  duniani. Hata hivyo, nchi imeghubikwa na vita vilivyokatili Maisha ya watu wengi kwa kwa karibu miaka mitano vikichochewa na ushindani wa kisiasa kati ya Rais Salva Kiir na naibu wake wa zamani, Riek Machar.

Viongozi hao wawili wametia saini mkataba wa Amani mjini, Sudan, jana Jumapili , makataba wenye lengo la la kutatua changamoto za utawala na kushirikiana madaraka mambo yanayohisiana na mkataba mwingine uliosainiwa Agosti 2015.

Akizungumzia hatua hiyo kutoka mjini Juba David Shearer, mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), amesema

SAUTI YA DAVID SHEARER

Mkataba huo ni hatua kubwa kusonga mbele katika kuleta amani Sudan kusini, wametia saini mkabata kuhusu utawala ambao kimsingi ni maandalizi ya anani atakayekuwa rais, nani watakaokuwa makamu wa Rais, kwa sababu watakuwa watano na pia kuunda bunge, hivyo ni hatua kubwa kwa upande huo.”

Lakini ambacho bado hakiko bayana ni

SAUTI YA DAVID SHEARER

Jinsi gani watapanga swala la  ulinzi kwa watu hao wote, na jinsi marekebisho ya ki mfumo kwa kuwajumuhisha wanamgambo katika jeshi, na mambo mengine ya kimaendeleo.  Huo utakuwa ni mwanzo mzuri ambao sote hatukutarajia miezi miwili iyopita.