Ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 ukiendelea kusambaa barani Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amependekeza hatua za kisera za kusaidia bara hilo kukabiliana na changamoto zitokanazo na janga hilo ambalo hadi sasa limesababisha vifo vya watu 2500 barani humo.
Kuelekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani tarehe 3 mwezi huu wa Mei, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wanahabari na wafanyakazi katika vyombo vya habari ni muhimu katika kusaidia ulimwenguni kupitisha maamuzi sahihi kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.
Waumini wa dini ya kiislamu ulimwenguni wakianza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa ujumbe wake wa kuwatakia heri katika mfungo wa sasa ambao amesema ni tofauti kabisa na mingine iliyotangulia kwa ajili ya janga la COVID-19.
Umoja wa Mataifa umesisitiza kwamba haki za binadamu zinapaswa kuwa muongozo katika hatua zinazochukuliwa kupambana na janga la mlipuko wa virusi vya corona au COVID-19.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ameelezea kugadhabishwa na kusikitishwa na mashambulizi yaliyotekelezwa na kundi la waasi la Taliban kwenye eneo la raia wengi lililopo mji mkuu wa Afghanistan, Kabul tarehe mosi mwezi huu wa Julai.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mkutano wa kundi la mataifa 20, G20 unafanyika wakati ambapo shaka na shuku zimekumba dunia nzima katika nyanja zote kuanzia kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Umoja wa Mataifa umeisihi dunia kushikamana na wakimbizi ambao wamelazimika kufungasha virago kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vita, mauaji , njaa na hata mateso kwani wanachokitaka ni amani.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye bado yuko ziarani nchini Fiji leo amekuwa na shughuli mbalimbali ikiwemo kuhutubia bunge la nchi hiyo, kuwa na mkutano wa pamoja na Waziri mkuu pamoja na kuzungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha South Pacific mjini Suva.