Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wamiliki wa mifugo Malakal wafurahia huduma kutoka kwa walinda amani

Walinda amani kutoka India wakipatia mifugo matibabu huko Sudan Kusini
UNMISS
Walinda amani kutoka India wakipatia mifugo matibabu huko Sudan Kusini

Wamiliki wa mifugo Malakal wafurahia huduma kutoka kwa walinda amani

Msaada wa Kibinadamu

Huduma za matibabu kwa wanyama zinazotolewa na walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini, zimeleta nuru kwa wakazi ambao wanategemea mifugo yao kwa ajili ya lishe na kujipatia kipato.  

Mjini Malakal jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini, mbuzi wakiswagwa kuelekea kituo cha matibabu ya wanyama.

Nyanawan Ayii ndio mmiliki ambapo matibabu hutolewa na walinda amani kutoka India wanaohudumu UNMISS.

Kituo hiki baada ya ukarabati kimeanza kazi mwezi Mei mwaka huu kikiendeshwa kama sehemu ya Chuo Kikuu cha Sayansi cha jimbo la Upper Nile. 

Ukarabati umewezesha walinda amani wa UNMISS kutibu wastani wa mifugo 200 kila wiki na Nyawan anaeleza kwa nini ameleta mbuzi wake kwa matibabu.

 “Natunza mbuzi wangu kwa sababu wananipatia maziwa ya kunywa na mengine nampatia mjukuu wangu. Ni chanzo cha utajiri wa familia yangu na ndio maana nimewaleta hapa kwa matibabu.”

Assumpta Massoi/UNNewsKiswahili
Kimfaacho mtu chake!

Sambamba na mbuzi, punda nao ambao hutumika kwa usafirishaji wanapatiwa matibabu hapa, mganga baada ya kumkagua punda na kubaini kuwa kamba aliyofungwa inamchubua na kumletea maumivu, akamdunga sindano.

Awali walinda amani walipita nyumba kwa nyumba kutibu mifugo lakini uwepo wa kituo hiki umesaidia huduma kutolewa hospitalini, na iwapo usalama utaimarika siku za huduma zitaongezwa badala ya sasa ambayo ni jumamosi pekee. 

Luteni Kanali Sengar ni daktari wa mifugo hapa Malakal

 “Serikali ya mtaa imeomba UNMISS iwapo hospitali hii ya wanyama inaweza kuongeza muda wa kufanya kazi ili mifugo iweze kutibiwa. WAnalalamika kuwa kuna magonjwa mengi na mifugo yao inakufa.”