Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bandari ya Mangala ni neema kwa Wasudan Kusini na wahudumua wa misaada:UNMISS

Mgao wa chakula huko Pieri nchini Sudan Kusini ambako WFP inasaidia watu 29,000 kati yao 6,600 ni watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano. (Picha 5 Februari 2019)
WFP/Gabriela Vivacqua
Mgao wa chakula huko Pieri nchini Sudan Kusini ambako WFP inasaidia watu 29,000 kati yao 6,600 ni watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano. (Picha 5 Februari 2019)

Bandari ya Mangala ni neema kwa Wasudan Kusini na wahudumua wa misaada:UNMISS

Msaada wa Kibinadamu

Kwa muda mrefu usafisrishaji wa mahitaji mbalimbali kwenye operesheni za mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS ambao unatumia aina mbalimbali za usafiri ukiwemo wa angani, barabara na majini kufikisha huduma lakini sasa kupitia bandari ya Mangala imekuwa rahisi kufikisha misaada inayohitajika kwa maelfu ya watu.

Katika bandari ya Mangala Sudan kusini maandalizi ya safari kupitia mto Nile yanafanyika UNMISS na mashirika na mengine ya Umoja wa Mataifa wamejaza shehena ya msaada  kupeleka sehemu mbalimbali inakohitajika. Kwa miaka 15 . Kwa miaka 15 nahodha Yor Oraj amekuwa akiendesha boti zinazobeba vifaa mbalimbali lakini tangu kuzuka vita Sudan kusini sasaanasafirisha misaada kama vile mafuta na chakula kwa ajili ya operesheni za UNMISS na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa likiwemo la mpango wa chakula WFP.

(SAUTI YA YOR ORAJ)

Kwetu sisi tunafanyakazi kwenye mto huu ili kuhudumia watu, pia tunabeba vifaa vya WFP kwa ajili ya kuwasaidia watu, kama tusipofanya kazi hii itakuwa shida kubwa kwa kaka zetu walio upande wa pili. Kama unavyoona kila kitu kinasafirishwa kutoka hapa kama vile mafuta na kupelekwa Malakal. Kila kazi ina umuhimu wake ya kwetu ni kubeba mafuta.”

 Vita viliposhika kasi Sudan Kusini vilifanya kuwa vigumu kusafirisha vitukupitia bandari hii  lakini sasa baada ya makaubaliano ya amani ya septemba 2018, hali ni shwari kwa safari za boti kama alivyoshuhudia kamanda wa vikosi vya UNMISS Luteni Jenerali Shailesh Tinaikar

(SAUTI YA SHAILESH TINAIKAR)

“Ni njia nafuu na ya haraka ambayo tunaimudu, ukizingatia changamoto za barabara na hali ya hewa Sudan Kusini, hivyo tuna boti ambayo inakwenda mara moja kwa mwezi na kubeba tani 2000-2500 katika kila safari na zinajumuisha mgao wa chakula na pia mafuta. Inachukua siku 10 hadi 12 kufika na siku zingine 15 kurejea .Ni operesheni muhimu sana kwa jeshi letu hivyo nimekuja na timu yangu kushuhudia na kujionea operesheni hii ngumu inavyofanyika na kuwasaidia kwa njia yoyote tuwezayo.”

Kwa UNMISS operesheni hii imeleta nuru sio tu kwa maelfu ya wanaohitaji msaada bali pia kurahisisha kazi ya wanaotoa misaada hiyo.