Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwezeshaji wa wanawake Afrika unahitaji maamuzi magumu na kuyatekeleza:Djinit

Wajumbe wa asasi za kiraia wakizungumza  na vyongozi wa Umoja wa Mataifa
UNMISS Photo
Wajumbe wa asasi za kiraia wakizungumza na vyongozi wa Umoja wa Mataifa

Uwezeshaji wa wanawake Afrika unahitaji maamuzi magumu na kuyatekeleza:Djinit

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Wakati wanawake barani Afgrika leo wakiadhimisha siku ya “Wanawake Afrika” iliyobeba kaulimbiu ‘’mtazamo na ubunifu” wamepongezwa kwa juhudi zao za kuchangia maendeleo barani humo.

Pongezi hizo zimetolewa na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya eneo la Maziwa Makuu Said Djinit akitoa wito wa kuweka msisitizo tena kwamba “uwezeshaji wa wanawake unahitaji sote kufanya maamuzi magumu na kuhakikisha utekelezaji wake hususani katika usawa wa kijinsia na haki za binadamu kwa wote.”

Mtazamo wa ofisi ya mjumbe huyo maalumu wa Maziwa Makuu ni kuhakikisha maendeleo ya wanawake katika ukanda huo na kuwafanya kuwa kama daraja katika kujenga Imani baina ya viungo mbalimbali vya jamii katika ngazi ya kitaifa na kikanda.

 

Mjumbe maalum wa katibu Mkuu ukanda wa Maziwa Makuu Said Djinnit akihutubia mkutanoni
UN Photo/JC McIlwaine
Mjumbe maalum wa katibu Mkuu ukanda wa Maziwa Makuu Said Djinnit akihutubia mkutanoni

 

Wadhamini wa amani , usalama na mpango wa ushirikiano kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ukanda mzima ambao ni Umoja wa Mataifa, muungano wa Afrika, ICGLR na ushirikiano wa kiuchumi kwa nchi za Kusini mwa afrika SADC, wanaendelea kupigia chepuo ushiriki wa wanawake katika ulingo wa siasa katika mchakato wa kufanya maamuzi yote na katika majadiliano yanayoendelea katika ukanda mzima wa Maziwa Makuu.

Amehimiza kwamba maadhimisho ya siku ya wanawake Afrika lazima pia yatumike kuhamasisha wajibu wetu wa kuchagiza ushirikiano na ubia wa kuleta suluhu ya kudumu katika changamoto za pamoja kama vile hali mbaya inayowakabili wanawake na watoto kila wakati kwenye makambi ya wakimbizi na wale wanaochukuliwa kama tegemezi kwenye makambi ya  wapiganaji wa zamani, uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake na ukosefu wa haki.

Ofisi ya mjumbe huyo maalumu inatoa wito kwa viongozi wa eneo la Maziwa Makuu wakati wakijiandaa kufanya mkutano wao wa 9 wa ngazi ya juu wa kikanda mjini Kampala Uganda baadae mwaka huu, kujizatiti tena katika kuunga mkono ushiriki wa kisiasa wa wanawake na kuwa vinara wa usawa wa kijinsia na haki za wanawake katika ukanda mzima.