Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlipuko wa Ebola kwaheri DRC: Tedros

Juni 20, mhudumu kutoka WHO anatoa chanjo kwa mwanaume nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC kijiji cha Bosolo
WHO/Lindsay Mackenzie
Juni 20, mhudumu kutoka WHO anatoa chanjo kwa mwanaume nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC kijiji cha Bosolo

Mlipuko wa Ebola kwaheri DRC: Tedros

Afya

Shirika la afya ulimwenguni WHO, kwa ushirikiano na wizara ya afya ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo   DRC, leo wametangaza rasmi kumalizika kwa  mlipuko wa Ebola katika jimo la Equateur nchini humo  baada ya jitihada za zaidi ya miezi miwili za kuudhibiti ugonjwa huo.

Akiwa ziarani nchini humo, mkurugenzi mkuu wa WHO Dk Tedros  Adhanom Ghebreyesus amepongeza jitihada za pamoja kati  ya shirika lake na  watalaam wa afya katika vituo mbalimbali vilivyo chini ya uratibu wa wizara ya afya nchini humo .

(Sauti ya DR Tedros Ghebreyesus)

"Leo tunakaribisha tamko kutoka kwa Waziri wa afya ya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa mlipuko wa  Ebola uliozuka nchini humu hivi karibuni umetokomezwa. Serikali ilichukua hatua haraka kukabilina na mlipuko huo,  na pia kukaribisha misaada ambayo inahitajika, na kuujulisha umma haraka kuhusuhatari ya ugonjwa huo. Aina hii ya uongozi huokoa maisha. Ninajivunia kazi ya WHO na washirika wake walioifanya katika kudhibiti  mlipuko wa Ebola. "

Watu kutoka shirika la msalaba mwekundu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakitoa mafunzo kuhusu maziko salama katika kijiji cha Itipo(Juni 10, 2018)
WHO/Lindsay Mackenzie
Watu kutoka shirika la msalaba mwekundu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakitoa mafunzo kuhusu maziko salama katika kijiji cha Itipo(Juni 10, 2018)

 

Na kuhusu mikakati ya shirika hilo katika kukabiliana na milipuko na majanga mengine yanayoikabili nchini hiyo Dk Tedros amesema

(Sauti ya DR Tedros Ghebreyesus)

"Kwa pamoja tunatakiwa  kukabiliana na milipuko mingine ambayo nchi inakabiliana nayo ikiwemo kipindupindu na polio. kwa pamoja tunatakiwa kuokoa zaidi ya watoto laki 3 ambao wanakufa kila mwaka kwa magonjwa yanayoweza kuepukika. Wizara ya afya ya DRC ilitangaza mlipuko wa Eboka mwezi mei mwka huu, na watu zaidi ya 20 wamepoteza maisha huku wengine takriban 50 waliugua kufuatia mlipuko huo katika  jimbo la Equateur nchini DRC"

WHO imetumia zaidi ya dola milioni 1.6 kutoka kwenye mkufo wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF kusaidia kudhibiti mlipuko huo huku wadau wengine wakiwemo shirika la Marekani la msaada wa nje wa majanga USAID, na serikali ya Italia wakitoa zaidi ya dola milioni 3 .

 

TAGS: DRC, Ebola, CERF, Dr. Tedros Ghebreyesus, WHO