Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tangu Juni 6 hakuna visa vipya vya Ebola DRC:WHO

Tarehe 5 Juni 2018, wahamasishaji wa kijamii huko DRC kwa usaidizi wa UNICEF walipita maeneo ya Mbandaka kuelimisha jamii ikiwemo watoto kuhusu jinsi ya kuepukana na Ebola
UNICEF/Mark Naftalin
Tarehe 5 Juni 2018, wahamasishaji wa kijamii huko DRC kwa usaidizi wa UNICEF walipita maeneo ya Mbandaka kuelimisha jamii ikiwemo watoto kuhusu jinsi ya kuepukana na Ebola

Tangu Juni 6 hakuna visa vipya vya Ebola DRC:WHO

Afya

Shirika la afya ulimwenguni WHO,  limesema limefanikikiwa kwa kiasi kikubwa  kuzuia mambukizi mapya na  kusambaa kwa ugonjwa wa ebola katika mkoa wa Mbandaka, nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC.

Tangu tarehe 6 juni mwaka huu , WHO inasema hakujaripotiwa kisa chcochote kipya ikiwa ni ishara ya mafanikio ya kudhibiti kuenea kwa mlipuko huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa WHO,Tarik Jasarevic amesema shirika hilo  kwa kushirikiana na shirika la madakitari wasio na mipaka MSF, walifanikiwa kuzuia maambukizi ya ebola kutokana na kampeni kubwa ya pamoja na utoaji wa  chanjo kwa zaidi ya watu 3,280.

Ameongeza kuwa, "mpaka sasa bado tuna visa vya watu 38 vilivyothibitishwa tangu tarehe sita ya mwezi june, na katika visa hivyo kuna maafa ya watu 28 na jumla ya visa ni 55. Bado tunaendelea kufuatilia kutokana na taarifa mbalimbali tunazozipata za watu ila wengi tuliowapima hawana maambukizi."

Ameongeza kuwa kwa sasa WHO inamalizia upimaji wa watu wengine 161  waliokuwa na uhusiano na wagonjwa  na zoezi hilo litakamilika hapo kesho tarehe 27 ili kubaini kama wana maambukizo au la.

Bw. Jasarevic amesema hii ni hatua nzuri katika kumaliza mlipuko wa ebola, ila bado wanafuatilia kwa karibu sana kuhahakikisha hakuna maambukizi yoyote au wagonjwa wapya jamhuri ya kidemokwasia ya Congo.

 WHO na washirika wote wataendelea kutoa usaidizi wa hali ya juu katika ufuatiliaji wa milipuko wa ebola duniani ili kutokomeza majanga ambayoyanazidi kukabili nchi masikini kote duniani.