Kashfa za ukatili wa kingono zinapungua- Lacroix

29 Disemba 2017

Mwaka 2017 ulikuwa wa majonzi makubwa kwenye operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa. 

Hiyo ni kauli ya Mkuu wa Idara ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix katika ujumbe wake wa kuhitimisha mwaka 2017.
Amesema walinda amani 60 wameuawa mwaka huu pekee wakati wakilinda amani lakini  hata hivyo…
 
(Sauti ya Jean-Pierre Lacroix) 
« Mwaka huu tumeweza kufunga ujumbe wetu huko Cote D’ivoire kwa kuwa jukumu letu lilifanikiwa na kukamilik, huko Haiti tumefunga ujumbe wetu na kuanzisha ujumbe mdogo sana wa kukidhi mahitaji  ya sas aya kusimamia utawala wa sheria. Na tuko karibuni kufunga ujumbe wetu huko Liberia. » 
Bwana Lacroix akaangazia changamoto walizokabiliana nazo ikiwemo ile ya tuhuma za kashfa ya ukatili wa kingono iliyokumba walinda amani. 
Amesema hivi sasa wametunga sera ya kukabiliana na ukatili wa kingono ambapo.
 
(Sauti ya Jean-Pierre Lacroix)
« Tunaweza kuona kuwa namba ya tuhuma zinapungua, na nchi zinazochangia askari zinachukua hatua, huku ripoti kuhusu tuhuma zinafika bila vikwazo. »

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter