Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Timu ya haki za binadamu ipelekwe Sudan kufuatilia kinachoendelea:OHCHR

Umati wa watu wakianadamana kwenye mitaa ya mji mkuu wa Sudan Kharthoum 11 Aprili 2019
PICHA:Ahmed Bahhar/Masarib
Umati wa watu wakianadamana kwenye mitaa ya mji mkuu wa Sudan Kharthoum 11 Aprili 2019

Timu ya haki za binadamu ipelekwe Sudan kufuatilia kinachoendelea:OHCHR

Haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa leo imependekeza kupelekwa haraka timu ya Umoja wa Mataifa ya waangalizi wa haki za binadamu nchini Sudan ili kufuatilia madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanyika tangu Juni 3 mwaka huu 2019.

Kwa mujibu wa ofisi hiyo ya haki za binadamu hali inayoendelea Sudan hivi sasa inatiwa hofu kubwa na kwamba hivi sasa ofisi hiyo inajaribu kupata ushirikiano wa serikali ili kufanikisha kupelekwa kwa timu hiyo ya Umoja wa Mataifa ambayo itataka kushirikiana na pande zote za mamlaka ya Sudan, mashirika ya asasi za kiraia na wadau wengine haraka iwezekanavyo. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu mjini Geneva Uswis

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

“Kwa mara nyingine tunatoa wito kwa uongozi kuhakikisha kunafanyika uchunguzi wa haraka, na huru wa matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya makundi ya waandamanaji ikiwa ni pamoja na madaikushirikisha msaada wa majeshi mengine ambayo miongoni mwa askari wake ni wapiganaji kwa kundi la wanamgambo wa zamani la Janjaweed lililohusihswa na ukiukaji  wa haki za binadamu kwenye jimbo la Darfur kati ya mwaka 2003 na 2008.”

Ameongeza kuwa uwajibikaji pia ni muhimu sana ili kuepuka umwagaji damu zaidi na kusisitiza haja ya kuwa na kipindi cha mpito chenye utulivu na kufuata utaratibu kuelekea utawala wa kiraia.