Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia Gaza; vituo vya afya vyazidiwa uwezo

Vituo vya afya vinakabiliwa na changamoto kufuatia ghasia ukanda wa Gaza
UNICEF/D'Aki
Vituo vya afya vinakabiliwa na changamoto kufuatia ghasia ukanda wa Gaza

Ghasia Gaza; vituo vya afya vyazidiwa uwezo

Msaada wa Kibinadamu

Wahudumu wa afya huko Gaza, Mashariki ya Kati hivi sasa wanahaha kutibu zaidi ya majeruhi 2700 wa ghasia za jana zilizosababisha vifo vya watu zaidi ya 58. Taarifa zaidi an Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

Umoja wa Mataifa umesema vituo vya afya vimezidiwa uwezo huku majeruhi wengine wakilazimika kuachwa kwenye veranda za hospitali kwa kuwa idadi ya wagonjwa ni wengi, na vifaa vya matibabu ni vichache.

Tarik Jasarevic ni msemaji wa shirika la afya ulimwenguni, Geneva, Uswisi.

(Sauti ya Tarik Jasarevic)

 “Uwezo wa huduma za afya Gaza ni mdogo sana na umekuwa ukikabiliwa na changamoto kubwa kwa zaidi ya miaka 10 ya migogoro inayoendelea ambapo ukosefu wa dawa na huduma za afya umekuwa kikwazo . mwezi huu kuna  aina  2 kati ya dawa 5 hazipatikani na nusu ya zilizosailia haina zaidi ya mwezi kuisha.  Dawa za huduma za dharura kama viuavijasumu( antibiatics) zinahitajita  

Nayo ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu ya umoja huo, OCHA imesema majeruhi 1,300 kati ya 2700 hao walishambuliwa kwa risasi za moto kutoka askari wa Israel.

Jens Laerke ni msemaji wa OCHA.

(Sauti ya Jens Laerke)

 “Mpaka hapo hakuna alipoteza maisha upande wa Israel, isipokuwa mwanajeshi mmoja wa aliyejeruhiwa na kupelekwa hospital kwa ajili ya matibabu. Baadaye tumepata taarifa ya kifo kimoja upande wa Israel.”

Naye mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Micheal Lynk amelaani kitendo hicho cha askari wa Israel kushambulia raia akitoa wito  kwa serikali ya Israel isitishe matumizi ya silaha za moto yasiyo ya lazima  kwa waandamanaji wa kipalestina  kwenye ukanda wa Gaza .