Afya kwa wote Afrika ni lazima ili kutimiza ajenda ya 2030

20 Aprili 2018

Ili kutimiza ajenda ya kimataifa ya maendeleo yaani SDG’s hapo mwaka 2030 hususani kwa mataifa ya Afrika, basi ni lazima kuhakikisha afya kwa wote inapatikana.

Hayo yamesemwa na Profesa Francis Omaswa mkurugenzi mtendaji wa kituo cha afya cha Afrika kwa ajili ya afya ya kimataifa na mabadiliko ya kijamii  nchini Uganda, anayehudhuria mkutano wa Dunia wa kikanda wa afya unaofanyika mjini Coimbra , Ureno.

Akizungumza na UN News kandoni mwa mkutano huo Profesa Omaswa amesema kikubwa walichijikita nacho ni

(SAUTI PROFESA OMASWA)

Naye Bi Monica Ferro mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu    UNFPA katika ofisi ya Geneva Uswisi amesema amewakilisha shirika lake kwenye mkutando huo ili kujadili umuhimu wa kuwekeza katika afya ya mwanamke  

(SAUTI YA MONICA FERRO)

Ni muhimu kuwekeza katika afya yao, ni muhimu kuwekeza katika upatikanaji wa uzazi wa mpango ili kuwapa fursa ya kupanga mwelekeo wa maisha ya baadaye  katika kupata elimu ya kutosha  ili  kuwapa  uwezo na ujasiri wa kuamua maisha yao ya baadaye na pia fursa ya ajira nzuri kama ilivyo kwenye mpango wetu wa kutomuacha  mtu yeyote nyuma.

Mkutano huo ulioandaliwa na shirika la afya duniani WHO, unakunja njamvi hii leo na umewaleta pamoja washiriki zaidi ya 100, mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa, asas iza kiraia na na wataalamu kkutoka Amerika, Ulaya, Asia , Amerika Kusini na Afrika ambayo imewakilishwa na takribani washiriki 100, ili kukuna vichwa na kutoka na mbinu za kuhakikisha lengo la afya kwa wote duniani linatimia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud