Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndio sisi ni Albino, hata mikate tukioka hamnunui?

Mawunyo Yakor-Dagbah, Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu nchini Ghana, GDF katika mahojiano na UN News jijini New York, Marekani.
UN News/Ben Malor

Haki za binadamu

Ulemavu wa ngozi bado unasalia kuwa kikwazo wa wahusika kujikwamua siyo tu kijamii bali pia kiuchumi. Hata hivyo nuru inaangazia kule ambako jamii yenyewe inachukua hatua.

Nchini Ghana kama ilivyo katika nchi nyingine za Afrika, kuwa na ulemavu wa ngozi au Albino ni kikwazo siyo tu cha kijamii bali pia kiuchumi, amesema Makamu wa Rais wa shirikisho la vyama vya walemavu nchini humo, Mawunyo Yakor-Dagbah. Siraj Kalyango.

(Taarifa ya Siraj Kalyango)

Huyu ni Mawunyo Yakor-Dagbah, jina lake Mawunyo likimaanisha Mungu ni mwema! Yeye ni mlemavu wa ngozi.

Na anasema Mungu amekuwa mwema kwake kwani ameweza kuvuka vikwazo kuanzia vya kielimu na kijamii hadi kuajiriwa katika ofisi ya Taifa ya ukaguzi wa hesabu nchini Ghana kama Mkaguzi mwandamizi.

Mawunyo Yakor-Dagbah, (kushoto) Makamu Rais wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu nchini Ghana, GDF akihojiwa na Assumpta Massoi wa UN News jijini New York, Marekani.
UN News/Ben Malor
Mawunyo Yakor-Dagbah, (kushoto) Makamu Rais wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu nchini Ghana, GDF akihojiwa na Assumpta Massoi wa UN News jijini New York, Marekani.

Mawunyo anasema ukiwa Albino hata uchuuzaji wa bidhaa ni tatizo kwa kuwa..

(Sauti ya Mawunyo Yakor-Dagbah)

“Baadhi yetu wamejifunza kuoka mikate. Watu wanawauliza, hivi ni wewe umeoka au unauza tu. Ina maana ukisema wewe ndio umeoka mtu anasema sinunui. Inasikitisha sana.”

Je nini muarobaini kwa Albino kuweza kupata ajira ?

(Sauti ya Mawunyo Yakor-Dagbah)

“Tunajaribu kusaka mafunzo ya kujitolea kazini. Mimi mwenyewe nilijifunzia ofisi ya taifa ya ukaguzi na baada ya mwaka mmoja niliajiriwa. Kwa uzoefu huo nadhani tunasaka mafunzo hayo kwa wanachama wetu na twatumai wataonyesha uwezo wao.”