Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

CSW62

UN News/Assumpta Massoi

Ukombozi wa mwanamke kijijini utategemea ushirikiswahi wake:FAO

Ili kuweza kumkomboa mwanamke wa kijijini, ni lazima ashirikishwe katika mchakato mzima, kuanzia utungaji wa sera hadi umilikaji wa ardhi.

Wito huo umetolewa na Bi Susan Kaaria afisa wa masuala ya jinsia katika idara ya sera ya shirika la chakula na kilimo FAO.

Katika makala hii anajadili na Flora Nducha, kama FAO wanafanya nini kufanikisha azma hiyo Ungana nao.

Sauti
3'9"
UN News/Selina Jerobon

Je redio za kijamii bado zina nafasi?

Radio za kijamii zina mchango mkubwa katika kumuendeleza mwanamke wa kijijini. Hiyo ni moja ya kauli zilizotanabaishwa wakati wa mkutano wa 62 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW uliomalizika hivi karibuni jijini New York, Marekani. 

Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo ni Marceline Nyambala,  Mkurugenzi Mkuu wa shirika la waandishi habari wa kike nchini Kenya, AMWIK,  ambaye ameelezea umuhimu wa redio za jamii wakati huu wa mitandao ya kijamii.

(Sauti ya Marceline Nyambala)

Sauti
1'53"
Wakazi wa Sangari Jamhuri ya Afrika ya kati wakisikiliza Radio Lego Tila Ouaka( Sauti ya Ouaka) redio ya jamii inawaleta pamoja waislamu na wakristo
Picha ya OCHA/Gemma Cortes

Je redio za kijamii bado zina nafasi?

Redio za kijamii zina mchango mkubwa katika kumuendeleza mwanamke wa kijijini. Hiyo ni moja ya kauli zilizotanabaishwa wakati wa mkutano wa 62 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW uliomalizika hivi karibuni jijini New York, Marekani. 

Sauti
1'53"
UN / Evan Schneider

Biashara yangu imevuka mipaka ya Tanzania- Lydia

Mkutano wa 62 wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW ukikunja jamvi hii leo jijini New York, Marekani, mmoja wa washiriki kutoka Tanzania Lidya Jacob amezungumzia mafanikio makubwa aliyopata katika kilimo na biashara hususan k wenye usindikaji wa bidhaa. John Kibego na ripoti kamili.

 Akihojiwa na Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa kando mwa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW62 jijini New York Marekani, Bi. Jacob amesema mafunzo ya usindikaji aliyopata yeye na wanawake wengine huko Kisarawe  yamewasaidia katika kukuza kilimo na biashara ya korosho.

Sauti
1'34"
UN News/Assumpta Massoi

Maji safi bado mkwamo kwa warendile huko Marsabit

Leo ni siku ya maji duniani ambapo Umoja wa Mataifa unapigia chepuo uhifadhi wa mazingira halisi ya eneo husika kama njia moja ya kukabiliana na uhaba wa maji duniani.

Wavuti mahsusi wa siku hii  unatambua mabadiliko ya tabianchi pamoja na uchafuzi wa mazingira na shughuli za kibinadamu kuwa moja ya sababu za uhaba wa maji.

Hatua pendekezwa za kudhibiti ni pamoja na kuhifadhi maeneo asilia kwa kupanda miti na kuhifadhi maeneo oevu.

Sauti
1'31"