Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la wanawake laendelea Sudan Kusini

Wanawake Sudan Kusini. Picha:Photo/JC McIlwaine

Kongamano la wanawake laendelea Sudan Kusini

Wanawake

Wakati kamisheni ya wanawake kutoka ulimwenguni kote, ya CSW62 ikiendelea jijini New York, mjini Juba nchini Sudan zaidi ya wanawake 150 wawakilishi wa jamii mbalimbali wamejumuika katika kongamano la kitaifa  la siku 3 kujadili amani na usalama nchini humo.

Kongamano hilo lililodhaminiwa na uakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNMISS, limesheheni viongozi na wawakilishi wanawake mbalimbali kutoka asasi za kiraia, vyombo vya usalama, serikali kuu na pia  uakilishi wa wakimbizi wa ndani ili kujali mustahabali wa amani na unyanyasaji wanaokabiliana nayo wanawake nchini humo.

Kutoka serikali ya Sudan ni Bi Lily Albino Akol ambaye katika huruba wake alisema…

(Sauti ya LILY)

Tunapoketi kama wanawake, tunapozungumza na tunaposhirikiana kimawazo, ni jambo la kupendeza, kwa sababu hii ndiyo njia pekee tunaweza kuchocgea mabadiliko. Ni wakati tunapokusanyika kama kikundi ndipo sauti zetu zinapoweza kusikia, na kuleta mabadiliko. "

Naye naibu mjumbe maluum wa katika mkuu nchini Sudan Moustapha Soumare aliyepata fursa ya kushirika kongamazo hilo la wanawake mjini Juba alisema…

(Sauti ya Moustapha Soumare)

Tumeona kwamba kupitia mchakato wa jukwaa hili, wanawake wameshirikiana na wamekuwa sauti moja, wamekuwa na nguvu ya  kuhamasisha uongozi katika ngazi tofauti nimelishuhudia nilipokuwa  Addis . Hapo awali kuna mara kadhaa ambako ilikuwa vigumu kuleta mabadiliko katika uongozi ila  walipoingia wanawake, jumuiya ya kiraia pamoja, wamefanikiwa kuleta mabadiliko. Lakini cha msingi ni kwamba zaidi, majadiliano haya ni zaidi ya jukwaa la uimarishaji, na ni zaidi kuleta amani too katika nchi hii.