Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zanzibar inasonga kuwawezesha wanawake vijijini: Fatma Bilal

Mradi wa nishati ya jua nchini Tanzania.(Picha:Benki ya dunia/video capture)

Zanzibar inasonga kuwawezesha wanawake vijijini: Fatma Bilal

Wanawake

Serikali ya Zanzibar imekuwa mfano wa kuigwa katika suala la uwezeshaji wanawake vijijini kujikwamua na umasikini kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo kama ilivyo  katika ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030. 

Taarifa kuhusu hatua hizo adhimu zimetolewa na Fatma Gharib Bilal, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, uwezeshaji wanawake na wazee ya serikali ya Zanzibar jijini New York, Marekani kando mwa mkutano wa 62 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW.

Bi.  Fatma akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumzia mradi wa umeme wa nishati ya jua ambao ni moja ya miradi iliyoanzishwa na serikali kwa ajili ya kuwawezesha wanawake wa vijijini huko Zanzibar.

(Sauti ya Fatma Gharib Bilal)

Na kuhusu ni vipi kupitia mradi huu uzalishaji na pia utengenezaji vifaa vya umeme wa nishati ya jua wanawake hao wa vijijini wananufaika pamoja na na kupata mafunzo,  Bi Fatma anasema..

(Sauti ya Fatma Gharib Bilal)