Tusaidie serikali kumkomboa mwanamke- Dkt. Soko
Wakati mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW62 ukiendelea jijini New York, Marekani wawakilishi wa mashirika ya kiraia kutoka Tanzania wamezungumziaumuhimu wa suala la uwezeshaji wanawake vijijini kupitia mafunzo mbalimbali waliyoyapata kwenye mkutano huu.
Mmoja wa wawakilishi hao ni Grace Soko Mkurugenzi Mtendaji chama cha wanawake wakristo Tanzania, YWCA, ambaye akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amesema kwa kuhudhuria CSW, amepata nafasi ya kubadilishana mawazo na mataifa mengine na pia kupata taswira ya dunia nzima kuhusu masuala ya wanawake, na kwamba….
(Sauti y a Dkt. Grace Soko)
Halikadhalika amesema YWCA katika ajenda zake, wamepatia kipaumbele suala la kupiga vita ukatili wa kingono dhidi ya wanawake nchini Tanzania ambapo wameongeza vituo vya usaidizi kwa wanawake katika kanda ya ziwa ambako visa vya ukatili dhidi ya wanawake vinazidi kuongezeka kila uchao.
(Sauti y a Dkt. Grace Soko)