#Metoo ni chachu ya kukomesha ukatili kwa wanawake: Bi Mohammed

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J Mohammed (Maktaba)
UN Photo/Manuel Elías
Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J Mohammed (Maktaba)

#Metoo ni chachu ya kukomesha ukatili kwa wanawake: Bi Mohammed

Wanawake

Mkutano wa kamisheni ya  hali ya wanawake duniani ,CSW62 unaendelea  mjini New York, ukisheheni mitazamo mbalimbali kutoka kwa washiriki akiwemo naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J Mohammed ambaye yuko mstari wa mbele kuunga mkono kampeni ya #Metoo ilizoanzishwa na wanawake Wakimarekani baada ya kubaini unyanyasaji wa kingono unaofanywa na wanaume wenye madaraka.

Bi Amina katika hotuba yake kwenye CSW 62 amesema kampeni ya #Metoo imechangia sana kuchochea mwamko katika harakati za kutetea haki na pia kupinga ukatili dhidi ya wanawanke sio tu marekani bali ulimwenguni kote….

Image
Uwezeshaji Wanawake utaboresha uchumi. Picha: UN Women

(Sauti ya Amina Mohammed.)

Kampeni ya MeToo ni  muhimu sana kwetu  kwa sababu hawa wanzilishi wamefanikiwa kujitolea  kwa sauti zao ili nasi tuchukukue jukumu la kukomesha ukatili kwa wanawake. Sio kwamba hatujafanya kazi hiyo. Lakini kila mara katika historia ya mwanadamu lazima watakuja mashujaa watakao shika nafasi ya mbele na baada ya hapo  ni lazima kuchukua fursa hiyo na kusonga mbele.

Kamisheni ya CSW62  itakayodumu kwa  wikii mbili imedhaminiwa na Umoja wa Ulaya EU iliyochangia kiasi cha Euro  laki 5, na inasimiwa na  mashirika ya Umoja wa Mataifa kama la maendeleo UNDP,  la idadi ya watu UNFPA na UN women  watakaotoa muongozo kuhusu miradi ya wanawake vijijini, kwa ushirikiano na  ofisi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.