Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana ni ufunguo wa mafanikio ya SDG’s:

Paschal Masalu   afisa mtendaji wa jukwaa la Elimikawikiendi  Tanzania akiwa katika kahojiano na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mtataifa jijini New York.

Vijana ni ufunguo wa mafanikio ya SDG’s:

Vijana wana mchango mkubwa katika kusongesha ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu au SDG’s . Hayo yamesisitizwa katika jukwaa la vijana la Umoja wa Mataifa 2018 lililokunja jamvi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja huo New York Marekani. Vijana 700 kutoka nchi mbalimbali wamejadili jinsi gani washirikishwe na mchango wao katika kufanikisha azma hiyo ya Dunia. Miongoni mwa waliohudhuria ni kijana Paschal Masalu kutoka nchini Tanzania ambaye ni afisa mtendaji wa jukwaa la Elimikawikiendi nchini humo. Amezungumza na Flora Nducha wa idhaa hii kuhusu yaliyojiri katika jukwaa hilo na hasa yapi aliyokuja kuyawasilisha kwenye jukwaa hili kutoka wa vijana wa kitanzania