Mashambulizi dhidi ya Rohingya ni jama za kuwatokomeza kabisa:UM

11 Oktoba 2017

Mashambulizi ya kikatili dhidi ya watu wa kabila la Rohingya yanayoendelea kaskazini mwa jimbo la  Rakhine yamethibititiswa kuwa ni jamaa zilizoandaliwa na waasi ili kuwafukuza Warohingya nje ya mipaka ya  Myanmar na kuwazuia kutorudi tena katika nchini hiyo.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo kuhusu ukiukwaji wa haki za binanadamu kwa wakimbizi wa kabila la Rohingya unaofanywa na  vikosi vya usalama vya Myanmar kwa kushirikiana na watu wenye silaha  wa dini ya Budda.

Ripoti hiyo imetokana na kukusanywa kwa maoani  kuanzia tarehe 14 hadi 24 septemba mwaka huu kutokana na mahojiano 65 yaliyofanywa kati ya ofisi ya haki za binadamu na warohingya na makundi mbalimbali,  ambapo msichana wa miaka 12 kutoka mji wa Rathedaung alielezea jinsi majeshi ya usalama wa Myanmar na watu wenye silaha wa dini ya Budda walivyozunguka nyumba yao na kuishambulia kwa risasi.

Naye Bw. Zeid Ra'ad Al Hussein Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja Mataifa  amsema mashambulizi yanaofanya na vikundi vya serilkali huko kaskazini mwa Myanmar ni mfano wa mauaji ya halaiki yenye lengo la kutokomeza kabila la wa Ronhingya na kuwanyima haki yao ya msingi ya kuishi na kujumuihswa katika siasa na uchmi wa nchi hiiyo.

Aidha hadi sasa kuna idadi ya Warohinhya 500,000 waliombilia Bangladesh tangu vikosi vya usalama vya Myanmar  vianzishe operesheni ya kukabiliana na mashambulizi dhidi yao  tarehe 25 Agosti 2017

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter