Jamii yachukua jukumu kulinda vyanzo vya maji Tanga, Tanzania

Jamii yachukua jukumu kulinda vyanzo vya maji Tanga, Tanzania

Athari za mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri katika jamii kufuatia matukio mbali mbali yanayoshuhudiwa.

Ni kwa mantiki hiyo ambapo baadhi ya jamii ya watu wa muheza mkoa wa Tanga nchini Tanzania wameamua kutunza mazingira kwa sababu hali ya kilimo, ufugaji na maji si nzuri kwao, na katika kulifahamu hilo wameunda umoja wao ujulikanao kwa jina la UWAMAKIZI yaani Umoja wa Wakulima wa Hifadhi Mazingira Kihugwi Zigi wakiwa na lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Radio washirika Voice of Africa ya mkoani Tanga imepata fursa ya kuzungumza na mwenyekiti wa umoja huo bwana Twaha Rajabu Mbarouk anayeanza kueleza sababu ya kuwepo umoja huo wa UWAMAKIZI.