Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vigezo vipya kwa wafanyabiashara kulinda watu wa LGBTI vyazindiliwa:UM

Vigezo vipya kwa wafanyabiashara kulinda watu wa LGBTI vyazindiliwa:UM

Kamishna Mkuu wa  haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein, leo amezindua vigezo vya aina yake vya kimataifa kwa ajili ya kusaidia wafanya biashara kukabiliana na ubaguzi dhidi ya watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, waliobadili jinsia, mashoga na wanawake wanaotembea na wanawake wenzao au LGBTI.

Kamishna Zeid, akizungumza na viongozi wa biashara, wanaharakati na waandishi wa habari katika makao makuu ya Microsoft jijini New York Marekani ametolea wito kwa sekta binafsi kuchukua nafasi yake katika kujumuisha kundi la LGBTI katika sehemu za kazi na kwingineko. Ameongeza kwamba mabadiliko katika jamii yanahitaji ushirikiano wa wote ikiwemo sekta ya biashara kwani maamuzi yao yanaweza kuathiri haki za binadamu.

Zeid ametaja vigezo vitano muhimu, mosi ni kuheshimu haki za binadamu za wafanyakazi wa kundi la LGBTI, wateja na umma, pili kutokomeza ubaguzi dhidi ya wafanyakazi wa kundi la LGBTI kazini, tatu kusaidia wafanyakazi wa LGBTI kazini, nne kuzuia ubaguzi na ukatili dhidi ya wateja, wauzaji na wasambazi wa bidhaa wa LGBTI, na tano simama kwa ajili ya haki za binadamu za watu wa kundi la LGBTI katika jamii ambako kampuni zinaendesha biashara.

Halikadhalika Kamishna Zeid amesema kutenga kundi lolote katika jamii kunaathiri wote katika jamii na kwamba kuondoa ubaguzi ndio ufunguo wa kukuza stadi na kuimarsiha uzalishaji.