Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usasa haujatowesha utamaduni wa ngoma ya Gwoka Guadeloupe

Usasa haujatowesha utamaduni wa ngoma ya Gwoka Guadeloupe

Visiwa vya Guadeloupe vinahakikisha kuwa ngoma yao iitwayo Gwoka inasongesha utamaduni ulioingia visiwani humo karne ya 17 wakati wa biashara ya utumwa. Gwoka ngoma ibebwayo kila kona za kisiwa hicho kinachomilikiwa na Ufaransa ni utambulisho wao wa karne na karne na sasa umeorodheshwa kwenye turadhi za tamaduni zisizogusika za shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi amekupeleka ulingoni.