Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa UM waonya kuhusu ongezeko la ubaguzi wa rangi Marekani

Wataalam wa UM waonya kuhusu ongezeko la ubaguzi wa rangi Marekani

Visa vya ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni vimeshamiri Marekani, kwa mujibu wa ripoti ya wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Onyo hilo limetolewa wakati huu ambapo maandamano na vurugu zimetanda katika mji wa Charlottesville jimbo la Virginia nchini marekani na mtu mmoja kupoteza maisha.

Kwa mujibu wa wataalam hao, maandamano hayo yanayotekelezwa na vikundi vya watu wenye misimamo mikali na chuki dhidi ya watu weusi yanasikitisha.

Katika mahojiano na Idhaa hii mmoja wa wataalam hao, mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu mifumo ya kisasa ya ubaguzi, ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na hali zingine za kutovumiliana, Mutuma Ruteere amesema..

(Sauti ya Ruteere)

Kwa hivyo...

(Sauti ya Ruteere)