Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia imetakiwa kutosahau ukatili wa ISIL dhidi ya Wayazidi

Dunia imetakiwa kutosahau ukatili wa ISIL dhidi ya Wayazidi

Miaka mitatu iliyopita mwezi huu kundi la kigaidi la ISIL lilishambulia mji waSinjar nchini Iraq, maskani ya Wayazidi walio wachache nchini humo na kuua raia na kuwafanya maelfu kukimbia.

Pia maelfu ya wanawake na wasichana wa jamii hiyo walitekwa na kupelekwa Syria walikolazimishwa kuingia katika utumwa wa ngono. Wengi wao bado wanashikiliwa hadi leo. Katika hafla ya iliyofanywa na mpango wa Umohja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI kukumbuka tukio hilo naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Iraq György Busztin amesema ukatili uliofanywa na ISIL dhidi ya kabila na dini ya Wayazidi walio wachache usisahaulike asilani.

(BUSZTIN CUT)

“Zahma ya wayazuidi ni kumbusho kwa watu wa Iraq , ukanda mzima na dunia kwa ujumla kwamba itikadi za chuki zisipodhibitiwa zinaweza kusababisha ukatili na unyama miongoni mwa wanyonge, wasio na ulinzi, na wasiojiweza miongoni mwao walio wachache.”

Katika kukumbuka ukatili huo wa Sinjar tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi kuhusu Syria imetoa wito wa kupatikana kwa haki dhidi ya Wayazidi, pia imezitaka pande zinazopigana dhidi ya ISIL kufikiria mipango ya kuwaokoa Wayazidi. Mwenyekiti wa tume hiyo ni Paulo Sergio Pinheiro..

(PINHEIRO-CUT)

“Wanapaswa kubainiwa ili waweze kukombolewa huo ndio ujumbe mkuu wa ombi letuili waweze kupata huduma za afya kwa sababu waliathirika vibaya sio tuu kimwili lakini pia kisaikolojia.”