Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzalishaji wa chuma cha pua warejea 2016:UNCTAD

Uzalishaji wa chuma cha pua warejea 2016:UNCTAD

Licha ya matumizi madogo nchini Uchina na gharama nafuu kwa takriban mwaka mzima sekta ya chuma cha pua imeshuhudia ongezeko la uzalishaji na usafirishaji nje wa bidhaa hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti mpyailiyotolewa leo na kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD , iitwayo “ripoti ya soko la chuma cha pua” sekta ya chuma cha pua imeshuhudia mabadiliko makubwa mwaka jana baada ya ukuaji mdogo, bei ya chini na faida kiduchu mwaka 2015.

Ripoti inaonyesha kwamba viashiria muhimu vya mahitaji na usambazaji, biashara na bei vyote viliongezeka kwa kipindi cha mwaka mzima na kulifanya soko la bidhaa hiyo kuimarika.

UNCTAD imeongeza kuwa soko la chuma ni muhimu sana katika uchumi wa dunia na miaka ya karibuni soko hilo liliyumba kutokana na sababu mbalimbali kama kutangazwa kwa hali ya dharura, na kudorora kwa uchumi katika nchi zinazoendelea.