Guterres alaani vifo vya Wapalestina watatu Jerusalem

21 Julai 2017

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vifo vya Wapalestina watatu vilivyotolea leo kwenye makabiliano na wanajeshi wa usalama wa Israel , na kutoa wito wa matukioa hayo kuchunguzwa. Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake , Guterres amesema fikra na sala zake ziko pamoja na familia za waathirika.

Katibu Mkuu ameongeza kuwa anatiwa hofu na machafuko yanayolipuka kwenye mji wa kale wa Jerusalem. Amewataka viongozi wa Israel na Palestina kujizuia na hatua zozote ambazo zitazidisha hali ya machafuko na kutoa wito kwa wanasiasa wote, viongozi wa dini na viongozi wa kijamii kusaidia kupunguza mvutano.

Katibu Mkuu amerejelea kauli kwamba maeneo matakatifu ya kidini ni lazima yaheshimiwe , kwa sababu ni mahala pa kutafakari na sio pa machafuko.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter