Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi DPRK acheni vitendo vinavyozorotesha hali ya sasa- Guterres

Viongozi DPRK acheni vitendo vinavyozorotesha hali ya sasa- Guterres

Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK leo imefanya jaribio la kombora la masafa marefu, kitendo ambacho kimeshutumiwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imemnukuu akisema kuwa kitendo hicho ni hatua nyingine ya ukiukwaji mkubwa wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Halikadhalika amesema kitendo hicho kinatishia hali ya kuzidi kuzorota kwa hali ya sasa.

Bwana Guterres amesema ni lazima viongozi wa DPRK wasitishe vitendo vya kuchochea hali ya hatari na wazingatie wajibu wao wa kimataifa.

Katibu Mkuu amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa kimataifa katika kupatia suluhu jambo hilo.