Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna hatua kubwa katika kupunguza hatari za silaha za maangamizi-UM

Kuna hatua kubwa katika kupunguza hatari za silaha za maangamizi-UM

Kuna hatua kubwa zilizopigwa na nchi wanachama katika miaka kadhaa iliyopita kwenye kupunguza hatari ya kuenea kwa silaha za maangamizi.

Hayo yamesemwa leo na Izumi Nakamistu mwakilishi wa ngazi ya juu katika idara ya upokonyaji silaha ya Umoja wa Mataifa akitoa taarifa kwenye baraza la usalama lililokuwa likijadili kudhibiti kuenea kwa silaha za maangamizi.

(SAUTI NAKAMISTU)

"Kuna hatua kubwa zimepigwa na nchi wanachama kupunguza hatari ya silaha za maangamizi hata hivyo tunazidi kushuhudia vitisho vipya na vilivyo vigumu zaidi katika suala hili”

Nakamistu amesema tunahitaji kufuatilia kwa karibu ukuaji wa haraka wa teknolojia na silaha za maangamizi katika mwenendo wa pamoja na wa kimataifa , na kisha kubaini hatua za kukabiliana na athari zake katika kupunguza hatari ya silaha za maangamizi.

(NAKAMISTU)

"Ingawa bado kuna vikwazo vigumu vya kiufundi kwa makundi ya kigaidi kuweza kutumia silaha za maangamizi, ongezeko la ukuaji wa teknolojia unaweza kufanya daraja hili kuwa rahisi kulivuka.”

Amesisitiza kwamba uratibu mzuri wa kimataifa na kubadilisha taarifa unaweza kuwa muhimu katika kusaidia kukabili changamoto hizi.