Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya Cyprus ni fursa ya kipekee, Guterres atiwa matumaini-UM

Mazungumzo ya Cyprus ni fursa ya kipekee, Guterres atiwa matumaini-UM

Mazungumzo mapya ya kuamua mustakhbali wa Cyprus yafanyika kwa muda wowote utakaohitajika lakini sio hakikisho kwamba yatazaa matunda amesema leo mpatanishi mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mchakato huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis, Espen Barth Eide amesema mazungumzo hayo sio nafasi ya miwsho ya kufikia muafaka baina ya upande wa Cyprus ya Ugiriki na Cyprus ya Uturuki lakini

(SAUTI YA ESPEN)

“Usifanye kosa, haitokuwa rahisi . Katibu Mkuu nami tuatafanya kila tuwezalo kusaidia, pia baraza la usalama ambalo limeshikamana katika mchakato mzima huu, hali kadhalika muungano wa Ulaya aambao unatoa msaada mkubwa, na taasisi zingine za kimataifa za fedha zinazohusika moja kwa moja. Hatahivyo hakuna miongoni mwetu atakayefanikisha hili kwa washiriki husika ni lazima wabebe jukumu na kujaribu kutumia fursa hii ambayo ninaiona ni ya kipekee .”

Ameongeza kuwa baada ya miongo ya mgawanyiko ulioanza 1974 hii ni fursa muhimu ya kuwa na mafanikio katika mazungumzo japo sio fursa ya mwisho ukizingatia mvutano uliopo katika kisiwa hicho cha Mediterranean.

Mpatanishi huyo amezikumbusha pande zote kiongozi wa Cyprus ya Ugiriki Nicos Anastasiades na yule wa Cyprus ya Uturuki Mustafa Akinci kwamba wote walichaguliwa kupitia tiketi ya muungano.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema anatiwa matumaini na kuanza kwa mazungumzo hayo ambayo pia atayahudhuria.

Umoja wa Mataifa utakuwepo kwenye mkutano huo kusaidia pande zote kupata muafaka ili makubaliano yanayomilikiwa na watu wa Cyprus yaweze kufikiwa.