Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda yapigwa jeki harakati dhidi ya ukatili wa kijinsia

Uganda yapigwa jeki harakati dhidi ya ukatili wa kijinsia

Benki ya dunia imeidhinisha dola milioni 40 kwa ajili ya miradi ya kukabili shida za kijamii na ukatili wa kijinsia nchini Uganda.

Fedha hizo ambazo ni mkopo wa masharti nafuu zitasaidia utekelezaji wa sera za miradi iliyoidhinishwa mwaka 2016 wakati huu ambapo ukatili wa kijinsia ikiwemo vipigo kutoka kwa wenzi wa ndoa vinaonekana ni jambo la kawaida.

Mwakilishi mkazi wa Benki ya dunia nchini Uganda, Christina Malmberg Calvo amesema Uganda imejaribu mbinu nyingi ambazo zimeonyesha mafanikio katika kupunguza ukatili wa kijinsia hasa watu kubadili tabia.

Hivyo amesema mradi huo utasaidia kuimarisha uwezo wa huduma za msingi ikiwemo mahitaji ya waathirika hasa yale ya kiafya.