Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Uchangiaji Damu, WHO inasema okoa maisha leo

Siku ya Uchangiaji Damu, WHO inasema okoa maisha leo

Leo ni Siku ya Kuchangia Damu Duniani , ambapo Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mwaka huu linalenga uchangiaji damu katika dharura, hususan kwa wale wanaotaka kusaidia. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Unaweza kufanya nini? Changia damu. Changia sasa. Changia mara kwa mara ", yenye kuhamasisha uchangiaji utakao kusanya damu na kuweka benki mapema ili kuokoa maisha pindi haja hiyo itakapoibuka.

WHO imesema mchango huo unahitajika zaidi katika bara la Afrika ambalo linaathirika sana na vita, milipuko ya magonjwa kama Ebola, ajali za bararani na majanga ya asili, ambayo yanaongeza mahitaji ya watu kuogezewa damu na changamoto za usafirishaji wake.

WHO inasema janga kubwa la kibinadamu la hivi sasa limeweka dhahiri upungufu mkubwa wa mfumo wa afya barani humo, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa damu kwa wakati muafaka na kwa usalama.

Hivyo katika maadhimisho haya WHO imesihi wadau husika kuimarisha mchango wa hiari, bila malipo, ili kuboresha benki ya damu salama na yenye kutosha kwa ajili ya dharura.