Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simulizi za wakimbizi wa ndani nchini Nigeria

Simulizi za wakimbizi wa ndani nchini Nigeria

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, watu zaidi ya milioni mbili katika maeneo ya bonde la ziwa Chad wamepoteza makazi yao kufuatia mashambuzizi ya Boko Haram. Wakimbizi na watu katika eneo hilo ikiwemo Nigeria wanahitaji msaada wa dharura, na makumi ya maelfu ya watoto wako hatari kupata magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa chakula bora. UNHCR inaongeza kuwa wanaume na wanawake pamoja na watoto hao pia wanahitaji ulinzi na usaidizi wa kisaikolojia baada ya kuvumilia vurugu za kutisha na unyanyasaji. Katika makala ifuatayo, Selina Cherobon anakutana na wakimbizi nchini humo. Basi ungana naye kusikiliza simulizi zao...