Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Babatunde afariki dunia

Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Babatunde afariki dunia

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA Babatunde Osotimehin, amefariki dunia. Amina Hassan na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Amina)

Nats..

Mwendazake Babatunde Osotimehin! Amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 68.

Raia huyu wa Nigeria, ameongoza UNFPA tangu mwaka tarere Mosi Januari mwaka 2011 akiwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Nne wa shirika hilo, hapa alikuwa anazungumzia umuhimu wa kuwalinda watoto wenye umri wa miaka 10.

Kufuatia taarifa hizo za kifo chake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia msemaji wake ameeleza masikitiko yake akituma salamu za rambirambi kwa familia, UNFPA na serikali ya Nigeria.

Amesema dunia imepoteza bingwa wa afya na ustawi wa wote na kwamba Dkt. Babatunde alipendwa na wengi kutokana na utetezi wake wa haki za wanawake na wasichana.

Hayati Babatunda kabla ya kuongoza UNFPA alikuwa waziri wa afya wa Nigeria.