Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlinda amani wa UNAMID auawa Nyala Sudan

Mlinda amani wa UNAMID auawa Nyala Sudan

Mlinda amani wa mpango wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNAMID ameuawa na kundi la watu wasiojulikana baada ya kuteka gari lao mjini Nyala jimbo la Darfur Kusini.

UNAMID imelaani vikali shambulio hilo ambalo ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.

Tukio hilo limeripotiwa kwa mamlaka ya Sudan na UNAMID imeitaka serikali ya nchi hiyo kuhakikisha inawakamata wahusika na kuwafikisha mbele ya sheria.

UNAMID pia imetuma salamu za rambirambi kwa familia ya mlinda amani huyo, walinda amani wenzie na serikali ya Nigeria atokako.