Afya ni suala la haki asema mkurugenzi mteule wa WHO Dr Tedros

24 Mei 2017

Mikakati yote lazima ihakikishe inaelekea kwenye fursa ya afya kwa wote, amesisitiza mkurugenzi mpya mteule wa shirika la afya duniani WHO akizungumza na waandishi wa habari Jumatano mjini Geneva Uswis.

Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambaye anapendelea kuitwa Dr Tedros  , anahimiza nchi wanachama kutoa huduma ya afya kwa wote na kutekeleza sheria na mikataba ya kimataifa ya afya .

Akielezea masuala ambayo atayapa kipaumbele , Dr Tedros amesema sababu ya kuanzishwa WHO 1948 bado ina uzito uleule hata leo hii,

(SAUTI DR TEDROS)

“Ambacho dunia ilikiahidi 1948 , afya kwa wote wakati WHO ilipoanzishwa bado ni sahihi hata leo, lakini bado nusu ya watu wote hawana fursa ya huduma za afya. Nadhani umewadia wakati wa kutimiza kauali zetu, na dunia nzima inalitaka hilo, kwamba afya ni suala la haki.

Mengine atakayoyapa kipaumbele ni jinsi WHO itakavyoshughulikia dharura za kiafya, kuleta mabadiliko na pia kurejesha imani ya wanachama kwa shirika hilo na kuhakikisha michango yao inatumika ipasavyo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter