Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatuwezi kutokomeza machafuko ya ugaidi kwa nguvu pekee-Bokova

Hatuwezi kutokomeza machafuko ya ugaidi kwa nguvu pekee-Bokova

Matumizi ya nguvu pekee hayatoshi kutowesha wimbi la machafuko yatokanayo na misimamo mikali, chuki kama vile dhidi ya wageni, ubaguzi wa rangi na ukosefu wa stahamala amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, Irina Bokova.

Bi Bokova ameyasema hayo katika hotuba yake ya kufungua mkutano wa nne wa jukwaa la dunia kuhusu majadiliano ya utamaduni unaoendelea mjini Baku nchini Azerbaijan.

Amesema stahamala imepungua miongoni mwa jamii, na mshikamano unahitajika,maelewano na heshima dhidi ya mchanganyiko wa watu.

Ameonya kwamba.

( Sauti Bokova)

‘‘Tunaona jamii zikifungiana milango, makundi madogo yakiteswa. Tunaona kuongezeka kwa chuki dhidi ya wazawa, chuki dhidi ya wayahudi, ubaguzi wa rangi, na ukosefu wa uvumilivu. Katika muktadha huu hatuna mbadala, lazima tusalie katika misingi ya kuheshimu haki za binadamu na utu.’’