Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kulinda misitu kuanzie mashinani: Thomson

Kulinda misitu kuanzie mashinani: Thomson

Mkutano wa 12 wa jukwaa la Umoja wa Mataifa kuhusu misitu umeanza leo mjini New York Marekani, ambapo utekelezaji katika ngazi ya mashinani wa mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kuhusu misitu kwa kipindi cha mwaka 2017 hadi 2030 umesisitizwa. Amina Hassan na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA AMINA)

Akizungumza katika mkutano huo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Peter Thomson amewaambiwa washiriki wa mkutano kuwa umuhimu wa misitu katika kulinda ustawi wa utu na mazingira hauna mjadala hususani katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Amesema mkakati wa Umoja wa Mataifa katika kulinda misitu umekuja wakati muafaka na kusema ili mkakati huu ufanikiwe lazima.

( Sauti Thomson)

‘‘Tupigie chepuo juhudi katika ngazi ya mtaa, kitaifa , kikanda na kimataifa ksaidai atumizi endelevu na ulinzi wa misitu ikiwamo kuwekeza katika kampeni za elimu za kukuza uelewa wa umuhimu wa misitu’’.

Rais wa Baraza Kuu kadhalika amesema jamii za watu wa asili zinapaswa kuzingatiwa na kutotengwa katika utekelezaji wa mikakati hiyo.