Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hata tukiondoka, kipindupindu kitatoweka Haiti- MINUSTAH

Hata tukiondoka, kipindupindu kitatoweka Haiti- MINUSTAH

Umoja wa Mataifa umesema mipango yake ya kufunga ujumbe wake wa kulinda amani nchini Haiti, MINUSTAH mwezi Oktoba mwaka huu, haitaathiri mikakati ya kutokomeza kipindupindu nchini humo.

Katika mahojiano maalum na redio ya Umoja wa Mataifa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti Sandra Honore ambaye leo amehutubia mjadala wa wazi wa baraza la usalama kuhusu Haiti, mikakati ya kutokomeza kipindupindu iliyoanzishwa na umoja huo ilikuwa shirikishi.

( Sauti Honore)

‘‘Umeshuhudia mikakati mipya iliyotangazwa na Katibu Mkuu mstaafu Ban mwezi Disemba mwaka jana, ambayo imeendelezwa na Katibu Mkuu Guterres ambaye mwanzoni mwa mwaka alitangaza changizo. Kazi hii inaendelea na matumaini yetu ni kwamba nchi wanachama zitaitikia.’’

Akizungumzia kimbunga Mathew kilichoathiri watu na miundombinu ya taifa hilo, amesema ikiwa ni miezi sita kabla ya kufungwa kwa MINUSTAH, mikakati ya ujenzi mpya wa Haiti imefanyiwa ugatuzi na hivyo ni endelevu.

MINUSTAH imekuwepo nchini Haiti kwa takaribani miaka 14 ambapo imeelezwa kuwa taifa hilo limeimarika katika sekta kadhaa ikiwemo usalama.