Umuhimu wa misitu ni dhahiri na hivyo inahitaji kulindwa

24 Machi 2017

Kila Machi 21, dunia haudhimisha siku ya misitu. Misitu ni uhai! Huu ni usemi ambao hutumika mara nyingi ukipigia chepuo umuhimu wa rasilimali hiyo ambayo huhifadhi maji, husaidia upatikanaji wa chakula, hewa safi na kwa ujumla mazingira bora kwa vizazi, hasa wakati huu ambapo uharibifu wa mazingira unaathiir mustakhbali wa sayari dunia.

Umuhimu huo ndiyo ulisukuma baraza kuu la Umoja wa Mataifa kutangaza rasmi siku ya kimataifa ya misitu, mnamo mwaka 2012. Maudhui ya mwaka huu ya maadhimisho ya siku hiyo ni misitu na nishati.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter