Ueledi ni msingi katika kufanikisha ulinzi wa amani

Ueledi ni msingi katika kufanikisha ulinzi wa amani

Umoja wa Mataifa umeazimia kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kingono vinavyotekelezwa na watendaji wake walio kwenye operesheni za ulinzi wa amani, iwe ni askari, polisi au watendaji wa kiraia.

Mratibu maalum wa Umoja huo katika kuimarisha hatua za chombo hicho dhidi ya ukatili wa kingono na unyanyasaji, Jane Holl Lutte amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa baada ya Katibu Mkuu kutangaza mikakati yake ya kutokomeza vitendo hivyo dhalimu.

Bi. Holl-Lutte amesema ueleni ni jambo muhimu na kuzingatia maadili ya Umoja wa Mataifa na kwamba..

(Sauti ya Jane)

“Tunafahamu watendaji weledi hawana uhusiano wa kingono na wateja wao au wasaidizi wao. unajenga mazingira ambapo kwayo watu wanahisi wanathaminiwa, halikadhalika mchango wao. Katibu Mkuu amebadili sera ya watoa siri ili watu wawe na imani kuwa iwapo watatoa taarifa basi hawatalipiziwa kisasi.”

Naye msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya operesheni mashinani, Atul Khare amesema jukumu kubwa la walinda amani ni kulinda raia.

(sauti ya Atul Khare)

“Walinzi hawawezi kuwa wauaji. Walinzi hawawezi kuwa wanyonyaji wa watu. Hivyo tunapaswa kuelimisha watu kuwa wakati wanawalinda hampaswi kukubali kuwa sehemu ya kile ambacho naita ukatili wa kingono au bila shaka ukatili na unyanyasaji. Na nadhani jamii kwa hili zinatusaidia.”