Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AFD yatoa mkopo wa Euro milioni 200 kwa IFAD kuwekeza maendeleo vijijini

AFD yatoa mkopo wa Euro milioni 200 kwa IFAD kuwekeza maendeleo vijijini

Wakuu wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo (IFAD) na shirika la maendeleo la Ufaransa (AFD) leo wametia saini muafaka wa kufanya kazi pamohja ili kuendelea maeneo ya vijijini ambao unajumuisha mkopo wa awali wa Euro milioni 200 kwa IFAD.

Akizungunmzia ushirika huo Rais wa IFAD Kanayo Nwanze amesema huo ni muafaka muhimu sana baina ya IFAD na ADF hasa katika wakati huu ambapo serikali linakabiliwa na changamoto nyingi kupata ufadhili wa maendeleo, na madai ya huduma ya IFAD yakiwa makubwa kuliko wakati mwingine wowote , hivyo ameongeza mkopo huo utatoa fursa kwa IFAD kuongeza uwekezaji vijijini kwa nchi zinzoendelea na kuzisaidia kufikia malengo ya maendeleo endelevu hasa ya kutokomeza njaa na umasikini ifikapo 2030.

Ufaransa imependa kuwa taifa la kwanza kuisaidia IFAD chini ya mpango mpya wa kukopa , kwa mwaka 2016-2018. Mashirika hayo mawili ymaeshawahi kushirikiana katika miradi mbalimbali ikiwemo uanzishaji wa mazao yanayohimili hali ya hewa na kusaidia mashirika ya wakulima Afrika.