Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Keating alaani shambulio la bomu Mogadishu:UNSOM

Keating alaani shambulio la bomu Mogadishu:UNSOM

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Michael Keating, amelaani vikali shambulio la mabomu katika maeneo mawili tofauti mjini Mogadishu yaliyoripotiwa kuuawa raia kadhaa na kujeruhi wengine wengi mapema Jumatatu.

Bwana Keating amesema bomu la kwanza limelipuka karibu na kituo cha mafunzo ya jeshi la taifa cha Dhagabadan, na taarifa za awali zikionyesha kwamba mtu wa kujitolea muhanga aliyekuwa akiendesha basi dogo lililosheheni vilupizi ndiye aliyekufa katika tukio hilo.

Shambulio la pili limefanywa pia na mtu wa kujitolea muhanga aliyekuwa anaendesha gari lililojaa vilipuzi na kugonga lango kuu la hotel ya Weheliye katika eneo lililokuwa na umati mkubwa watu barabara ya Makka al-Mukarama kwa makusudi ya kutaka kuua idadi kubwa ya watu hasa wahudumu wa hoteli, wageni na wapiti njia.Kundi la kigaidi la Al-Shabaab limedai kuhusika na uhalifu huo.