Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IMF yajadili usaidizi wake Gambia

IMF yajadili usaidizi wake Gambia

Ujumbe wa shirika la fedha duniani, IMF ukiongozwa na Ulrich Jacoby umehitimisha ziara yake ya wiki moja huko Gambia, ziara iliyolenga mazungumzo kati ya taasisi hiyo na serikali mpya iliyoingia madarakani mapema mwaka huu.

Akizungumza mwishoni mwa ziara hiyo iliyoanza tarehe 16 mwezi huu Bwana Jacoby amesema mazungumzo yao na viongozi mbali mbali akiwemo Rais Adama Barrow, wadau wa maendeleo na sekta binafsi, yalijikita katika maendeleo ya kiuchumi na changamoto zake pamoja na vipaumbele vya maendeleo vya serikali.

Ujumbe huo umeshukuru ushirikiano ambao Gambia imeonyesha wakati wa ziara hiyo, ukisema mashauriano yalikuwa ni ya wazi na kwamba wanasubiri kwa hamu majadiliano zaidi yaliyopangwa kufanyika wiki chache zijazo yakiangazia usaidizi wa IMF kwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.