Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yahamisha watu 6000 kutoka Wau Sudan Kusini

IOM yahamisha watu 6000 kutoka Wau Sudan Kusini

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeendelea kuboresha maisha ya wakimbizi wa ndani katika maeneo ya ulinzi wa raia yaliyorundikana mjini Wau Sudan Kusini.

Likiwa linahifadhi wakimbizi wa ndani zaidi ya 30,000 , Wau ambalo linatazamana na kituo cha umoja wa Mataifa ni moja ya kambi iliyona na msongamano mkubwa nchini Sudan Kusini.

Sasa kwa ushirikiano na uongozi wa kambi hiyo IOM imefanya zoezi la kuhamisha zaidi ya wakimbizi wa ndani 6000, tangu Januari 26 mwaka huu , na kuwapeleka katika makazi mengine 800 ya jamii . Katika makazi hayo mapya familia zinaendelea kupokea huduma muhimu kama vile kliniki za afya zinazoendeshwa na IOM na madaktari wasio na mipaka MSF.