Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN-HABITAT yatunukiwa kwa utatuzi wa migogoro DR Congo

UN-HABITAT yatunukiwa kwa utatuzi wa migogoro DR Congo

Shirika la makaazi la Umoja wa Mataifa UN-HABITAT limekabidhiwa tuzo na jamii ya Mahagi iliyo kwenye wilaya ya Ituri mashariki mwa Congo kutokana na juhudi zake za kutafuta amani na utatuzi wa mizozo ya ardhi.

Uamuzi wa ni nani angenyakua tuzo hilo ulifanywa na wazee wa wilaya ya Ituri , utawala wa wilaya , wasomi , waandishi na wasikilizaji wa radio. Tuzo hilo limeitambua UN-HABITAT kutokana na jitihada zake za kuzuia mizozo kwa njia ya amani inayotokana na umiliki wa ardhi kwa kutoa hamasisho na kupitia kwa mapatano.

UN-HABITAT imekuwa ikiendesha shughuli zake wilayani Ituri kwa muda wa mwaka mmoja uiiopita ikishirikiana na wunyeji kutoka maeneo ya Djukoth, Angh'al, War' Palar na Mahagi katika utatuzi wa mizozo ya ardhi ikiwa na lengo la kuziwesesha jamii hizi kuishi kwa amani.