Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Andrew Gilmour alaani hali ya kutisha ya haki za binadamu Sudan Kusini

Andrew Gilmour alaani hali ya kutisha ya haki za binadamu Sudan Kusini

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Andrew Gilmour amelaani hali ya haki za binadamu nchini Sudan Kusini baada ya ziara yake ya siku nne nchini humo akisema wale wanaofanya uhalifu na ukatili huo lazima kuwajibishwa. Rosemary Musumba na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ROSE)

Bwana Gilmour amesema ukatili na ukiukwaji umefanywa dhidi ya wanaume, wanawake na watoto wa Sudan Kusini na njia pekee ya kuukomesha ni wahusika kuwajibika kisheria kwa kile wanachokifanya.

Gilmour amefanya mikutano mjini Juba na mawaziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, waziri wa habari, mkuu wa wafanyakazi kwenye SPLA, mkurugenzi mkuu wa jeshi la la usalama wa taifa, wawakilishi wa tume ya haki za binadamu nchini humo, washirika wa Umoja wa Mataifa na wahudumu wa kibinadamu, mashirika yasiyo ya kiserikali, viongozi wa mitaa, na wa dini, waathirika na watendaji vyama vya kiraia, pia alipata fursa kuzuru Malakal, ambapo alipata maelezo zaidi kuhusu mateso ya raia katika eneo hilo.

Bwana Gilmour amesema hii ikiwa ni mara yake ya nne kuzuru Sudan Kusini tangu mwaka 2011, hajawahi kuona uharibifu kama unaoendelea Malakal ikiwemo ukiukwaji wa wazi wa haki za binadamu, na mateso ya watu. Bwana Gilmour ametoa wito pande zote kupambana na vitendo hivyo vya ukatili hata kama ni wakati wa vita.